Description
Stadi za Kiswahili – Shughuli za Lugha – Kitabu cha Mwanafunzi, Gredi ya Tatu ni kitabu cha kiada cha Kiswahili kilichoandaliwa kwa kufuata Mtaala wa Kiumilisi.Kitabu hiki kina sifa kuu zifuatazo:
- Kinatumia Kiswahili cha kiwango cha mwanafunzi wa Gredi ya Tatu.
- Kinatumia maswali dadisi kukuza umilisi wa uwazaji wa kina na utatuzi wa matatizo
- Kinajumuisha shughuli za mwanafunzi akiwa peke yake,akiwa na wenzake na akiwa na wenzake katika kikundi
- Kinajumuisha mada na mada ndogo zote zilizomo katika mtaala wa Kiswahili wa kiwango hiki
- Yaliyomo yanawasilishwa kwa ubunifu wa kiwango cha juu
- Kinashughulikia matokeo yote maalum yanayotarajiwa kwa mujibu wa mtaala wa kiwango hiki
- Kinajumuisha umilisi wa kimsingi kwa mujibu wa mtaala wa Kiswahili wa Gredi ya Tatu.
- Kinakuza maadili kwa mujibu wa Mtaala wa Kiswahili wa Gredi ya Tatu.
- Shughuli za ujifunzaji zinakuza stadi za Kuskiliza na Kuzungumza,Kusoma na Kuandika pamoja na Sarufi.
Hayo na mengine mengi yanadhamiriwa kumwezesha mwanafunzi wa Gredi ya Tatu kutumia Kiswahili sanifu katika mazingira mbalimbali.
Reviews
There are no reviews yet.