Description
Kiswahili Chanana, Kitabu cha Mwalimu, Gredi ya Kumi ni kitabu kilichoundwa kwa dhamira ya kumwezesha mwalimu kufanikisha ujifunzaji wa yaliyomo katika Kiswahili Chanana, Kitabu cha Mwanafunzi, Gredi ya Kumi. Mwalimu anaelekezwa jinsi ya:
-
kutumia maswali dadisi ili kumfikisha mwanafunzi,
-
kukuza umilisi na mtagusili kulingana na mada ndogo mbalimbali,
-
kuyuanganisha masuala mtambuko katika mada ndogo mbalimbali,
-
kubuni mbinu na vifaa vya kutathmini kazi ya mwanafunzi baada ya kushughulikia kila mada ndogo,
-
kubaini mbinu mwafaka za ujifunzaji kwa kuzingatia upekee wa mwanafunzi,
-
kutambua mahitaji maalum ya kielimu na jinsi ya kuwashughulikia wanafunzi wenye mahitaji hayo,
-
kuandaa na kutunz nyenzo za ujifunzaji,
-
kujiandaa ifaavyo ili kufanikisha vipindi vya somo la Kiswahili.
Hayo na mengine mengi yanadhihirisha kumwezesha mwalimu kufanikisha vipindi vya Kiswahili.





