Description
Ouma, amka. Kuna nini? Mbona huamki? “Saa za kwenda shuleni zimefika,” alisema babake Ouma. Baada ya kuugongagonga mlango kwa muda hakusikia chochote.
Wazazi wake Ouma walimwambia mmoja wa wafanyakazi auvunje mlango wa chumba cha Ouma.
Mlango ulipovunjwa, kila mmoja alipigwa na butwaa; Ouma hakuwa mle ndani.Dirisha la chumba chake pia lilikuwa wazi….
Barua ya Maisha ni kutabu usichoweza kukiacha hadi usome hadithi nzima.Hadithi hii itawasisimua wasomaji kwa jinsi ilivyosimuliwa kwa ufundi mkubwa.





