Description
CBC Breakthrough Workbook Kiswahili, Gredi ya 6 ni kitabu cha mazoezi kilichoandikwa kwa ubunifu ili kumpa mwanafunzi nafasi ya kujitathmini. Mazoezi yaliyomo yametungwa kutokana na mada ndogo za Kiswahili Gredi ya 6 kulingana na mtaala wa kiumilisi. Kupitia kitabu hiki, mwanafunzi atahusishwa:
-
kuyadurusa mambo muhimu aliyojifunza katika vitabu vya kiada vya Kiswahili vya kiwango hiki kwa kuzirejelea sehemu za Mazingatio
-
kutathmini kiwango chake cha umilisi kwa mujibu wa mtaala wa kiumilisi
-
kuziimarisha stadi za lugha: Kusikiliza na Kuzungumza, Kusoma na Kuandika
-
kusoma vifungu vya kusisimua vinavyoangaza masuala mtambuko na maadili
-
kutumia lugha ya Kiswahili kwa usahihi katika mawasiliano yake ya kila siku
-
kujifunza kutokana na mazingira na jamii yake
-
kutumia vifaa vya kiteknolojia ili kuimarisha umilisi wa ujuzi wa kidijitali
-
kuimarisha uwezo wake wa uwazaji kina na utatuzi wa matatizo.
Haya na mengine mengi yanadhamiwa kumpa mwanafunzi wa Gredi ya 6 msingi imara wa ujifunzaji wa somo la Kiswahili.





