Description
Hatua za Kwanza, Mazoezi ya Lugha, Kiwango cha Kwanza cha Chekechea ni kitabu cha kiada kilichoandikwa kwa mujibu wa Mtaala wa Kiumilisi. Kitabu hiki kina sifa zifuatazo:
-
kinafunza shughuli za lugha kupitia kwa picha maridadi
-
kinatumia lugha sahili na mwafaka kwa mwanafunzi
-
kina shughuli za ujifunzaji za aina mbalimbali
-
kinamwezesha mwanafunzi kujifunza lugha kutokana na mazingira yake
-
kinashughulikia matokeo yote maalumu katika mtaala kwa kuzingatia umilisi wa kimsingi, madai na masharti ya mtaala mkuu
-
kinakuza stadi za kusikiliza na kuzungumza, kusoma na kuandika
Hayo na mengine mengi yanakusudiwa kumwezesha mwanafunzi wa Kiwango cha Kwanza cha Chekechea kuwa na stadi za kimsingi za lugha.





