Description
Hazina Bora
Mwandishi: Walibora
ISBN: 9789966342515
Baada ya Fatuma kuanguka kutoka juu ya mwembe wa Mzee Mataka, Matufu, Matule na Msilangu wanasingiziwa kuwa ndio waliomwangusha. Wanatoroka kijiji cha Bombani kuukwepa mkono mrefu wa sheria. Wanadhamiria kwenda kijiji cha Wendapole ambako wakazi wake wanasemekana kuwa wakarimu.
Safari yao inakumbwa na tatizo la kwanza — ngalawa wanayoiiba kutorokea inaingia maji na kuzama baharini. Wanatapatapa na kuogelea kwa shida ili kunusuru roho zao. Hata wanapofaulu kufika upande wa pili, hali inaendelea kuwa ngumu. Wanakumbwa na kadhia na misukosuko isiyo na kikomo. Je, hatima ya watoro hawa itakuwaje?





