Description
Karani na ndugu zake wanaandamana na wazai wao kwenda shambani.Wanapofika shambani, Karani anajitenga na wengine na kwenda kuketi chini ya mwembe.
Baadaye,Karani anaondoka shambani bila yeyote kumuona.Anakwenda nyumbani na kuchukua ndoana yake na kikapu na kuelekea mtoni kuvua samaki.Karani anabahatika kuwavua samaki wawili na kuwaweka kikapuni,nyuma yake.Samaki hao wanatoweka kimuujiza.Je, ni nani anayewaiba samaki hao?Masaibu yake hayakuishia hapo…….





