Description
Stadi za Kiswahili Gredi ya 7 – Kitabu Cha Mwalimu
Stadi za Kiswahili ni mfululizo wa vitabu vya kiada vya Kiswahili vilivyoandaliwa kwa kufuata Mtaala wa Kiumilisi.Kitabu hiki,Stadi za Kiswahili,Kitabu cha Mwalimu,Gredi ya 7,kinadhamiriwa kumwezesha mwalimu kufanikisha ufunzaji wa yaliyomo katika Stadi za Kiswahili,Kitabu cha Mwanafunzi,Gredi ya 7.Mwalimu anaelekezwa jinsi ya:
- kutumia maswali dadisi ili kumfikirisha mwanafunzi
- kukuza umilisi kulingana na mada ndogo mbalimbali
- kubaini uhusiano wa mada ndogo mbalimbali na masuala mtambuko
- kukuza maadili kulingana na mada ndogo mbalimbali
- Kubuni mbinu za kutathminia umilisi walioupata wanafunzi baada ya kushughulikia matokeo maalum yanayotarajiwa katika mada ndogo mbalimbali.
- kubaini mbinu mwafaka za ufunzaji.
- kutambua mahitaji maalum ya kielimu na jinsi ya kuwashughulikia wanafunzi wenye mahitaji hayo.
- kutayarisha nyenzo za ufunzaji
- kujiandaa ifaavyo ili kufanikisha vipindi vya somo la Kiswahili
Haya na mengine mengi yanadhamiriwa kumwezesha mwalimu kusimamia ifaavyo vipindi vya somo la Kiswahili kwa mujibu wa Mtaala wa Kiumilisi.
Reviews
There are no reviews yet.