Stadi za Kiswahili- Kitabu cha Mwalimu Gredi ya 6

Original price was: KShs597.40.Current price is: KShs538.24. inc. VAT

Stadi za Kiswahili- Kitabu cha Mwalimu Gredi ya 6 AUTHOR : Mwalimu Kipande ISBN : 9789966633453

Category:
Tags:

Description

Stadi za Kiswahili ni mfululizo wa vitabu vya kiada vya Kiswahili vilivyoandaliwa kwa kufuata Mtaala wa Kiumilisi. Kitabu hiki, Stadi za Kiswahili, Kitabu cha Mwalimu, Gredi ya 6, kinadhamiriwa kumwezesha mwalimu kufanikisha shughuli zilizomo katika Stadi za Kiswahili, Kitabu cha Mwanafunzi, Gredi ya 6. Mwalimu anaelekezwa jinsi ya:

  • kubaini umilisi unaokuzwa katika mada ndogo mbalimbali

  • kubaini uhusiano wa mada ndogo mbalimbali na masuala mtambuko

  • kubaini uhusiano wa mada ndogo mbalimbali na masomo mengine

  • kutambua maadili yanayokuzwa katika mada ndogo mbalimbali

  • kutambua shughuli za kijamii zinazochangia ujifunzaji katika mada ndogo mbalimbali

  • kubuni mbinu za kutathminia umilisi walioupata wanafunzi baada ya matokeo maalum yanayotarajiwa katika mada ndogo mbalimbali

  • kubaini mbinu mwafaka za ujifunzaji

  • kutambua mahitaji maalum ya kielimu na jinsi ya kuwashughulikia wanafunzi wenye mahitaji hayo

  • kutayarisha nyenzo za ufundishaji na ujifunzaji

  • kujiandaa ifaavyo ili kufanikisha vipindi vya somo la Kiswahili.

Haya na mengine mengi yanadhamiriwa kumwezesha mwalimu kusimamia ifaavyo vipindi vya somo la Kiswahili kwa mujibu wa Mtaala wa Kiumilisi.

Additional information

ISBN

9789966633453

Author

Mwalimu Kipande

Select at least 2 products
to compare