Description
Stadi za Kiswahili, Mwongozo wa Mwalimu, Gredi ya Saba ni kitabu ambacho kiliandikwa kwa dhamira ya kumwezesha mwalimu kufanikisha ufunzaji wa yaliyomo katika Stadi za Kiswahili, Kitabu cha Mwanafunzi, Gredi ya Saba. Mwalimu anaelekezwa jinsi ya:
-
kutumia maswali dadisi ili kumfikirisha mwanafunzi,
-
kukuza umilisi kulingana na mada ndogo mbalimbali,
-
kubaini uhusiano wa mada ndogo mbalimbali na masuala mtambuko
-
kukuza maadili kulingana na mada ndogo mbalimbali,
-
kubuni mbinu kutathminia umilisi wa mwanafunzi baada ya kushughulikia matokeo maalum yanayotarajiwa katika mada ndogo mbalimbali,
-
kubaini mbinu mwafaka za ufunzaji,
-
kutambua mahitaji maalum ya kielimu na jinsi ya kuwashughulikia wanafunzi wenye mahitaji hayo,
-
kutayarisha nyenzo za ufunzaji,
-
kujiandaa ifaavyo ili kufanikisha vipindi vya somo la Kiswahili.
Haya na mengine mengi yanadhamiriwa kumwezesha mwalimu kusimamia ifaavyo vipindi vya somo la Kiswahili kwa mujibu wa Mtaala wa Kiumilisi.





