Description
Author: Alfred Kibandi Gakuru
ISBN : 978 9966 63 293 7
Stadi za Kiswahili ni mfululizo wa vitabu vya kiada vya Kiswahili vilivyoandaliwa kwa kufuata Mtaala wa Umilisi. Kitabu hiki kina sifa kuu zifuatazo:
- Kimeandikwa kwa Kiswahili cha kiwango cha mwanafunzi wa Gredi ya 5.
- Maswali dadisi yametumiwa kutanguliza dhana zilizomo.
- Kimejumuisha shughuli za mwanafunzi binafsi,shughuli za wanafunzi wawiliwawili na za makundi ya wanafunzi.
- Kimeshughulikia masuala makuu yote kwa mujibu wa ruwaza ya Kiswahili cha Gredi ya 5.
- Kimejumuisha mada kuu na mada ndogo zote.
- Yaliyomo yamepangwa kulingana na ruwaza ya Kiswahili cha Gredi ya 5.
- Yaliyomo yamewasilishwa kwa ubunifu wa kiwango cha juu.
- Kimeshughulikia matokeo maalum yanayotarajiwa katika Gredi ya 5.
- Kimejumuisha masuala mtambuko yote.
- Yaliyomo yanakuza maadili yanayopendekezwa katika Mtaala wa Umilisi.
- Shughuli za ujifunzaji zinakuza stadi za kusikiliza na kuzungumza,kusoma na kuandika.
- Michoro na picha za rangi zinachangia yaliyomo kueleweka kwa urahisi.
- Maandishi makubwa na ya rangi mbalimbali yanayosomeka kwa urahisi.
Haya na mengine mengi yanadhamiriwa kumwezesha Mwanafunzi wa Gredi ya 5 kuwasiliana kwa Kiswahili sanifu katika mazingira mbalimbali.
Reviews
There are no reviews yet.