Description
Stadi za Kiswahili ni mfululizo wa vitabu vya kiada vya Kiswahili vilivyoandaliwa kwa kufuata Mtaala wa Kiumilisi.
Kitabu hiki kina sifa kuu zifuatazo:
ā¢ Kimeandikwa kwa Kiswahili cha kiwango cha mwanafunzi wa Gredi ya 9
ā¢ Maswali dadisi yametumiwa kumfikirisha mwanafunzi
ā¢ Kimejumuisha shughuli za mwanafunzi binafsi, shughuli za wanafunzi wawiliwawili na za makundi
ā¢ Kimejumuisha mada na mada ndogo zote
ā¢ Yaliyomo yamepangwa kulingana na mpangilio wa Kiswahili Gredi ya 9
ā¢ Yaliyomo yamewasilishwa kwa ubunifu wa kiwango cha juu
ā¢ Kimeshughulikia matokeo maalum yanayotarajiwa katika Gredi ya 9
ā¢ Kimejumuisha umilisi wa kimsingi kwa mujibu wa Mtaala wa Kiumilisi
ā¢ Kimeshughulikia masuala mtambuko yote
ā¢ Yaliyomo yanakuza maadili yanayopendekezwa katika Mtaala wa Kiumilisi
ā¢ Shughuli za ujifunzaji zinakuza stadi za Kusikiliza na Kuzungumza, Kusoma na Kuandika.
Haya na mengine mengi yanadhamiriwa kumwezesha mwanafunzi wa Gredi ya 9 kuwasiliana kwa Kiswahili sanifu katika mazingira mbalimbali.