Description
Stadi za Kiswahili ni mfululizo wa vitabu vya kiada vya Kiswahili vilivyoandaliwa kwa kufuata Mtaala wa Kiumilisi. Kitabu hiki kina sifa kuu zifuatazo:
-
Kimeandikwa kwa Kiswahili cha kiwango cha mwanafunzi wa Gredi ya 6.
-
Maswali dadisi yametumiwa kutanguliza dhana zilizomo.
-
Kimejumuisha shughuli za mwanafunzi binafsi, shughuli za wanafunzi wawiliwawili na za makundi ya wanafunzi.
-
Kimeshughulikia masuala makuu yote kwa mujibu wa mpangilio wa Kiswahili Gredi ya 6.
-
Kimejumuisha mada kuu na mada ndogo zote.
-
YaliyoYomo yamepangwa kulingana na mpangilio wa Kiswahili Gredi ya 6.
-
YaliyoYomo yamewasilishwa kwa ubunifu wa kiwango cha juu.
-
Kimeshughulikia matokeo maalum yanayotarajiwa katika Gredi ya 6.
-
Kimejumuisha umilisi wa kimsingi kwa mujibu wa Mtaala wa Kiumilisi.
-
Kimeshughulikia masuala mtambuko yote.
-
Yaliyomo yanakuza maadili yanayopendekezwa katika Mtaala wa Kiumilisi.
-
Shughuli za ujifunzaji zinalingana na stadi za Kusikiliza na Kuzungumza, Kusoma na Kuandika.
-
Michoro na picha za rangi zinachangia yaliyomo kueleweka kwa urahisi.
-
Maandishi makubwa na ya rangi mbalimbali yanasomeka kwa urahisi.
Haya na mengine mengi yanadhamiriwa kumwezesha mwanafunzi wa Gredi ya 6 kuwasiliana kwa Kiswahili sanifu katika mazingira mbalimbali.





