Description
Stadi za Kiswahili ni mfululizo wa vitabu vya kiada vya Kiswahili vilivyoandaliwa kwa kufuata Mtaala wa Kiumilisi. Kitabu hiki kina sifa kuu zifuatazo:
-
Kimeandikwa kwa Kiswahili cha kiwango cha mwanafunzi wa Gredi ya 7
-
Maswali dadisi yametumiwa kumfikirishia mwanafunzi
-
Kimejumuisha shughuli za mwanafunzi binafsi, shughuli za wanafunzi wawiliwawili na za makundi ya wanafunzi
-
Kimejumuisha mada na mada ndogo zote
-
Yaliyomo yamepangw ang kulingana na mpangilio wa Kiswahili Gredi ya 7
-
Yaliyomo yamewasilishwa kwa ubunifu wa kiwango cha juu
-
Kimeshughulikia matokeo maalum yanayotarajiwa katika Gredi ya 7
-
Kimejumuisha umilisi wa kimsingi kwa mujibu wa Mtaala wa Kiumilisi
-
Kimeshughulikia masuala mtambuko yote
-
Yaliyomo yanakuza maadili yanayopendekezwa katika Mtaala wa Kiumilisi
-
Shughuli za ujifunzaji zinakuza stadi za Kusikiliza na Kuzungumza, Kusoma na Kuandika.
Haya na mengine mengi yanadhamiria kumwezesha mwanafunzi wa Gredi ya 7 kuwasiliana kwa Kiswahili sanifu katika mazingira mbalimbali.