Stadi za Kiswahili – Shughuli za Lugha – Gredi 2

Original price was: KShs315.00.Current price is: KShs284.00. exc. VAT

Stadi za Kiswahili, Kitabu cha Mwanafunzi, Gredi ya 2 ni kitabu cha kiada kilichoandaliwa kwa mujibu wa mtaala mpya uegemeao umilisi uliozinduliwa na Taasisi ya Ukuzaji Mitaala ya Kenya (KICD) mnamo Septemba 2017. ISBN : 978 9966 63 030 8 Author : Mwalimu Kipande

Description

Stadi za Kiswahili, Kitabu cha Mwanafunzi, Gredi ya 2ni kitabu cha kiada
kilichoandaliwa kwa mujibu wa mtaala mpya uegemeao umilisi uliozinduliwa na
Taasisi ya Ukuzaji Mitaala ya Kenya (KICD) mnamo Septemba 2017. Kitabu hiki
kimejumuisha mada zote kuu na ndogo zilizomo katika ruwaza ya mtaala ya
Kiswahili cha Gredi ya 2. Isitoshe, mada kuu na ndogo zimepangwa kulingana na
jinsi zilivyopangwa katika ruwaza hiyo.
Fauka ya haya, yaliyomo yamewasilishwa kwa ubunifu wa hali ya juu ili kuyaoanisha
na umilisi wa kimsingi, masuala mtambuko, maadili miongoni mwa masuala
mengine yanayofumbatwa na mtaala mpya uegemeao umilisi.
Kitabu hiki kimejumuisha shughuli za aina nyingi za kufanywa na mwanafunzi
binafsi, wanafunzi wawiliwawili na makundi ya wanafunzi. Kazi na shughuli za
wanafunzi wawiliwawili na wanafunzi katika makundi zinadhamiriwa kuimarisha
stadi za kusikiliza na kuzungumza na vilevile umilisi wa ushirikiano na mawasiliano.
Aidha, kitabu hiki kimesheheni vifungu vya kusoma na vya kuchangamsha
vitakavyomsaidia mwanafunzi kuimarisha stadi ya kusoma. Stadi ya kuandika
haijaachwa nyuma. Kitabu kinazo shughuli za kutosha za mwanafunzi ili kustawisha
stadi ya kuandika.
Kwa mintarafu hii, kitabu hiki kitamwezesha mwanafunzi wa Gredi ya 2 kuwasiliana
kwa Kiswahili sanifu katika mazingira mbalimbali yanayoshughulikiwa katika mada
kuu.

Additional information

Weight 0.3 kg

Reviews

There are no reviews yet.

Only logged in customers who have purchased this product may leave a review.