Description
Author: Alfred Kibandi Gakuru
ISBN : 978 9966 63 294 4
Stadi za Kiswahili ni mfululizo wa vitabu vya kiada vya Kiswahili vilivyoandaliwa kwa kufuata Mtaala wa Umilisi. Kitabu hiki, stadi za Kiswahili,Kitabu cha Mwalimu,Gredi ya 5,kinadhamiriwa kumuwezesha mwalimu kufanikisha mafunzo yaliyomo katika Stadi za Kiswahili,Kitabu cha Mwanafunzi,Gredi ya 5.Mwalimu anaelekezwa jinsi ya:
- kubaini Umilisi unaokuzwa katika mada mbalimbali
- kubaini uhusiano wa mada mbalimbali na masuala mtambuko
- kubaini uhusiano wa mada mbalimbali na masomo mengine
- kutambua maadili yanayokuzwa katika mada mbalimbali
- kutambua shughuli za kijamii zinazochangia umili walioupata wanafunzi baada ya matokeo maalum yanayotarajiwa katika mada mbalimbali
- kubaini mbinu mwafaka za ujifunzaji
- kutambu mahitaji maalum ya kielimu na jinsi ya kuwashughulia wanafunzi wenye mahitaji hayo
- kutayarisha nyenzo za ufundishaji na ujifunzaji
- kujiandaa ifaavyo ili kufanikisha vipindi vya somo la Kiswahili
Haya na mengine mengi yanadhamiriwa kumwezesha mwalimu kusimamia ifaavyo vipindi vya somo la Kiswahili kwa mujibu wa Mtaala wa Umilisi.
Reviews
There are no reviews yet.