Description
Stadi za Kiswahili,Kitabu cha Mwanafunzi, Gredi ya Nne ni kitabu cha kiada cha Kiswahili kilichoandikwa kwa kufuata Mtaala wa Kiumilisi.Kitabu hiki kina sifa kuu zifuataza:
- Kinatumia Kiswahili cha kiwango cha mwanafunzi wa Gredi ya Nne.
- Kinatumia maswali dadidi kukuza umilisi wa uwazaji wa kina na utatuzi wa matatizo.
- Kinajumuisha shughuli za mwanafunzi akiwa peke yake,akiwa na wenzake na akiwa na wenzake katika kikundi.
- Kinajumuisha mada na mada ndogo zote zilizomo katika mtaala wa Kiswahili wa kiwango hiki
- Yaliyomo yanawasilishwa kwa ubunifu wa kiwango cha juu
- Kinashughulikia matokeo yote maalum yanayotarajiwa kwa mujibu wa mtaala wa kiwango hiki
- Kinajumuisha umilisi wa kimsingi kwa mujibu wa mtaala wa Kiswahili wa Gredi ya Nne
- Kinashughulikia masuala mtambuko kama inavyoelekezwa katika Mtaala wa Kiswahili wa Gredi ya Nne
- Kinakuza maadili kwa mujibu wa Mtaala wa Kiswahili wa Gredi ya Nne
- Shughuli za ujifunzaji zinakuza stadi za Kusikiliza na Kuzungumza, Kusomana Kuandika pamoja na Sarufi.
Hayo na mengine mengi yanadhamiriwa kumwezesha mwanafunzi wa Gredi ya Nne kutumia Kiswahili sanifu katika mazingira mbalimbali.
Reviews
There are no reviews yet.