Description
Ndoto ya Almasi
Mwandishi: Ken Walibora
ISBN: 978 9966 34 232 4
?…Almasi kadhalika aliitafuta redio kuukuu ya baba?ake iliyokuwa imekwisha kazi. Akaifumua na kuifanyia marekebisho sikwambii kuwatimua mende na buibui waliokuwa wameigeuza maskani yao …”
Almasi ni kijana mwenye ndoto. Ndoto kubwa. Ana bidii kama mchwa na ukakamavu unaomithilishwa na ule wa tai anayerarua dhoruba za upepo na kupaa juu mawinguni. Je tai huyu ataweza kufikia kileleta cha ndoto yake akiwa anaishi kwenye nchi yenye jinamizi la kutisha la ukabila? Nchi ambayo ukabila umejenga ghorofa, ukabila umenunua ndege, ukabila umetengeneza barabara.
Mbali na ukabila pia ni nchi yenye sheria za mnyonge mnyongeni?
Ndoto ya Almasi ni riwaya yenye changamsho na changamoto.Itamchesha msomaji…naam, na kumliza pia. Ndoto ya Almasiinatumia mbinu kalikali za fasihi. Stihizai yake ni kali kama pilipili manga na chungu kama shubiri. Msomaji atagundua kwamba riwaya hii haihusu hatima ya ndoto ya Almasi tu bali inahusu ndoto za watu wengi wanoishi katika nchi nyingi zinazoendelea.
Reviews
There are no reviews yet.