Description
Shani na Zani waliitika kwa kutingisha vichwa vyao, kisha wakakunja magoti na kutega masikio. Pazia la kitendawili kilichowazuga wakazi wa mji huo kwa miaka na mikaka sasa lilianza kufunguka taratibu.
“Nguva wa Shimoni ana jina jingine la siri. Wakazi wengi wa mji huu hawalijui. Pengine hata baba yangu halijui maana sijawahi kumsikia akilitaja.” Babu Bonga akaanza kusimulia hadithi hiyo kwa udondozaji stadi.
“Wazee wachache walioluka chumvi kama mimi wanalifahamu jina hilo. Amepewa jina hilo kutokana na maumbile na hulka yake. Vivyo hivyo, kutokana na mahali pale anapoibukia. Inasemekana nguva huyo ana siri moja inayo fungamana na utajiri mkubwa ajabu. Je, mme wahi kulisikia jina lake la pili?”
Vitabu vingine katika mfululizo huu:
-
Miujiza ya Majini
-
Pepo za Mizimu
-
Sokwe wa Milima ya Mwezi




