Description
Njozi Yapata Mtenzi
ISBN: 978 9966 63 170 1
Mwandishi: Mwenda Mbatiah
Njozi Yapata Mtenzi ni riwaya ambayo ina simulizi yenye mikondo kadha inayoingiliana. Mkondo mkuu unamhusu Kiguto ni kijana hodari masomoni, jamali wa sura na mwana wa jadi kubeli. Ana vipawa na nafasi nyingi za kujiendeleza maishani, ikiwa ni pamoja na kujiunga na chuo kikuu cha nchini au cha ng’ambo. Anapojiunga na mafunzo ya polisi – kazi inayodharauliwa, anawashangaza wengi. Sababu yake ya kufanya hivyo ni kufuata ndoto yake. Je, atatimiza ndoto hiyo au ataambulia patupu?
Hii ni riwaya inayotumia mbinu na mikakati anuwai kumzindua msomaji kuhusu changamoto na manufaa ya uhuru wa kimawazo. Inawafunza vijana kwamba wanaweza kuibadilisha mitazamo hasi ya wanajamii kuhusiana na baadhi ya taaluma na ajira. Kuweza kufanya hivyo, kunahitaji ndoto kuu na ujasiri mkubwa wa kuzifanikisha. Mitindo ya riwaya ya upelelezi, ya kijasira na ya kijamii imetumiwa sawia kuwasilisha yaliyomo.
Reviews
There are no reviews yet.