Description
Mfalme alihisi ng’ambo za masikio yake zikidunda, zikiparibika kupasuka kutokana na mchagizo wa milio mikali ya mizimu nje ya madhabahu. Ndani aliona viuvi vya mizuka miwili ikirukaruka na kumzunguka yule mwana, mmoja ameshika kigongo. Halafu akaanza kuona miujiza.
Toka kiononi hadi kichwani, umbo la mwana huyo likaumbuka na sura yake ikang’ong’onea. Manyoya yakaota nusu ya mwili wake. Viuvi vya mizuka vikazidi kuchafuka kama viempandwa na mizimu. Yule mwana mara akageuka sokwe mtu.
Ndani ya kitabu hiki, msomaji ametunukiwa hadithi nyingine ya kusisimua iliyo na anwani, “Mbuyu wa Serengeti”.
Vitabu vingine katika mfululizo huu:
-
Nguva wa Shimoni
-
Pepo za Mizimu
-
Miujiza ya Majini




