Description
Uchambuzi wa Damu Nyeusi na Hadithi Nyingine
Author: Walubengo Mendi
ISBN: 978 9966 345 92 9
Uchambuzi wa Damu Nyeusi na Hadithi Nyingine ni kitabu kilichoandaliwa kukidhi mahitaji ya uchambuzi wa hadithi fupi kwa wanafunzi wa shule za upili. Kila hadithi katika mkusanyiko wa hadithi fupi Damu Nyeusi na Hadithi Nyingine imechambuliwa kwa kuzingatia vigezo na dhana muhimu. Aidha, maelekezo muhimu kuhusu jinsi ya kujibu maswali ya mikondo mbalimbali yamejumuishwa.
Maelekezo yaliyotolewa katika kitabu hiki yanadhamiriwa kuchochea na kuongoza fikra za mwanafunzi ili apate kuelewa kwa undani hadithi husika.
Mwanafunzi, kwa hivyo, asijibane tu katika maelezo yaliyotolewa bali maelezo hayo yawe kama mwanga wa kumwezesha kuona mambo mengine yaliyofichama katika hadithi.
Reviews
There are no reviews yet.