Description
Jamii ya Magofu ikiwemo Shule ya Upili ya Magofu inakabiliwa na uozo katika kila fani ya maisha. Si ufisadi, si ulevi na utumiaji wa mihadarati, si uharibifu wa mazingira….. Karibu kila fani inaminywa na jeshi la wawi. Jeshi hilo linapania kuidumisha hali hiyo ili liendelee kujinufaisha. Mazingira hayo magumu yanachochea kuibuka kwa jeshi la wema lenye ari na uthubutu wa kutaka mabadiliko. Makabiliano makali yanatokea kati ya majeshi ya pande hizo mbili. Je, jeshi la wema litafaulu katika azma ya kutakasa fani mbalimbali za jamii ya Magofu? Tamthilia hii inasawiri mapambano ya wema na uovu katika jamii yoyote ambayo inahangaikia mabadiliko chanya.





