Description
“Ukungu wa ndoto ulifungua pazia.
Adamu akajiona pale ufukoni akiwa bado na kijana wake. Ziwani aliona viuvi viwili vikibuka, vikatamba na kuwang’ong’olea. Baada ya nukta mbili tatu, aliona madege mawili yakirandaranda angani. Majini kuluzuka kivuli cha ngangarika. Kivuli hicho kilikuwa si kigeni. Mara akasikia mayowe yakimka,
‘Mianzi ya pua!’
Adamu alizinduka kutoka usingizini akikariri, ‘Mamba mla watu!’ huku jasho jembamba likimchuruzika usoni.” Adamu alikurupuka kitandani, akangazia huku na kule kama kwamba bado alikuwa ndotoni. Dirishani, mwangaza wa alfajiri ulipepua. Mara alihisi mguso ukimshika na kumtikisa.
Vitabu vingine katika mfululizo huu:
-
Ngwa wa Shimoni
-
Pepo za Mizimu
-
Sokwe wa Milima ya Mwezi




